JAVA

Monday, November 16, 2015

DIAMOND PLATNUMZ NA VANESSA MDEE WAFANYA MAAJABU KWENYE TUZO ZA AFRIMA



Weekend iliyopita zilifanyika tuzo za muziki za All African Music Awards 2015 maarufu kama AFRIMA Awards zilitolewa usiku wa jumapili wa November 15 Lagos, Nigeria 
ambapo wa Tanzania wawili Diamond Platnumz na Vanessa Mdee walifanikiwa kunyakua tuzo hizo.
Kwenye tuzo hizo Diamond Platnumz alifanikiwa kupata tuzo tatu na Vee Money akafanikiwa kupata tuzo moja. 
Diamond Platnumz alikuwa anawania vipengele vitatu mwaka huu kwenye tuzo za AFRIMA Awards 2015 ambavyo vyote aliibuka mshindi, ‘Artist of the year kilichokuwa kinawaniwa pia na Alikiba, Davido, Wizkid, Yemi Alade, Jose Chameleone, Flavour na SarkodieBest Male Artist in East Africa pamoja na Song of The Year ambapo wimbo wa Nasema Nawe uliibuka kuwa wimbo bora wa mwaka.
Vanessa Mdee amefanikiwa kupata tuzo ya Best African Pop kupitia hit single yake ya  Hawajui.



No comments:

Post a Comment