linex
baba levo
sumalee
Mchana wa jana Msanii wa bongo fleva Linex aliongea live kwenye Bongo Rhymes ya mwambao fm Tanga na Hansy Vipaji kuhusu ajali waliyoipata wakielekea kigoma jana . oLinex amesema hawakuwa kwenye mwendo wa kasi kwani show zao ni weekend so mwendo wao ulikuwa mdogo sana na ndio maana haikuwa ajali kubwa .Dancer mmoja wa Suma lee ameumia Mguu na Gari la Suma Lee ndio lililoumia sana upande wa mbele,kwani taa zimepasuka na sehemu ya mbele kuharibika sana. Ajali ilisababishwa na basi la abiria lililokuwa katikati ya barabara kwenye kona kali, ambapo ili kulikwepa lazima Suma angetakiwa atoke nnje ya barabara, ndipo gari ilipomshinda na kugonga mti .Linex ,Baba levo na Suma lee wana show tatu weekend hii Ijumaa mjini Kigoma , Jumamosi ni Kasulu na Jumapili ni Bujumbura. Thank God Wako Poa.
No comments:
Post a Comment