JAVA

Wednesday, August 29, 2012

MARTINI KADINDA ATAWAKA MAJUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!!!


MBUNIFU mahiri wa kitanzania, Martin Survivor Kadinda ‘Martin Single Button’ anatarajia kuonyesha mavazi yake kesho nchini Marekani katika onyesho la mavazi la New York Africa Fashion Week na Music on The Caltwalk.
Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema Martin atakuwa huko pamoja na wabunifu wengine saba kutoka sehemu mbalimbali za Afrika.
“Martin ni mmoja wa wabunifu ambao wamechaguliwa kushiriki kwenye onyesho hilo, litakaloambatana na utoaji tuzo kwa wasanii wa filamu na wanamuziki wengine wa Nigeria.”
Mbali na makoti maarufu ya Single Button, Martin ataonyesha pia nguo zake mpya ziitwazo vibunduki pamoja Kivumbi Collection ambazo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwenye Dar Fashion Festival.
Akizungumzia nafasi ya kushiriki onyesho hilo, Kadinda alisema amefurahia kwa kuwa itampa nafasi ya kukutana na wabunifu wengine wakubwa duniani na kujifunza mambo mbalimbali katika sanaa.
“Hii ni changamoto kubwa kwangu, nitaitumia vizuri kuhakikisha naongeza ujuzi katika sekta ya ubunifu, nashukuru kwa maandalizi ambayo One Touch wamefanya kwa ajili ya kunikutanisha na watu mbalimbali nchini Marekani watakaonipa malekezo juu ya kazi yangu,” amesema.
Music on the Catwalk itafanyika ukumbi wa Hellen Mills Event & Theater mjini New York. MOC ni onyesho la kila mwaka ambalo limebuniwa kwa ajili ya kukuza vipaji vya wasanii wa muziki pamoja na mavazi ambapo lengo kuu ni kutangaza kazi za wasanii wa Kiafrika.
Kwa mara ya kwanza Music on the Catwalk ilifanyika mwaka 2008, ambapo mbunifu Ally Rehmtullah ndiye alishiriki kwa mara ya kwanza katika onyesho lililofanyika Uingereza ambapo pia alipata nafasi ya kuhudhuria London Fashion Week.
Kampuni ya True Media ya Uingereza ndio waandaji wa maonyesho hayo wakishirikiana na Nigeria Entertainment Awards (NEA) ambapo One Touch Solutions ndio wawakilishi wa kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki. Onyesho kama hilo linatarajiwa kufanyika pia Uingereza mwezi Novemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment