Baada ya kufanya mahojiano na kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio rapper kutoka kundi la Weusi Joh Makini amefunguka juu ya gharama alizozitumia wakati wa
kushoot video yake mpya ya Don't Bother ambayo ameifanya South Afrca na director Justin Compos.
"Video ya Don’t Bother Ft rapa AKA aliyofanya na muongozaji Justin Campos wa kampuni ya Gorrilla Films ya Afrika Kusini imegharimu jumla ya dola 15000 ambazo ni sawa ya milioni 32 za Kibongo" - Joh Makini
Pia aliongezea kwa kusema kuwa wimbo wa Don’t Bother umevunja rekodi ya nyimbo zake zote kwa kutrend Tanzania na nje zaidi na kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment