JAVA

Friday, October 9, 2015

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA LIVERPOOL BAADA YA ROGERS KUTIMULIWA


 Jurgen Klopp anakabiliwa na mtihani wa kuirudisha Liverpool katika chati yake ya kuwa tishio ulaya baada ya kusaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa misimu mitatu
.
Liverpool wamemsajili kocha huyo baada ya kumtimua kazi aliyekuwa kocha wao Brendan Rodgers kuinoa timu hiyo  kwa misimu miwili iliyopita bila ya mafanikio.
Klopp ambaye alijiuzulu kuifundisha Borrusia Dortmund msimu uliopita anatarajiwa kutambulishwa leo kwa vyombo vya habari mara baada ya kusaini mkataba jana Alhamisi.
Katika hali isiyo ya kawaida, klabu ya Borrusia Dortmund kupitia ukurasa wake wa Twitter imemtakia kila la kheri kocha huyo katika maisha yake mapya na Liverpool.
Dortmund walipost picha ya mjerumani huyo huku wakimtakia kila lenye heri. Liverpool nao waliwajibu wenzao wa Dortmund kwa furaha waliyokua nayo kwa kupokea ujumbe huo.
Kocha huyo sasa ataanza mtihani wake wa kwanza dhidi ya Tottenham Hotspur weekend ijayo katika mchezo wa ligi kuu England ugenini White Hart Lane.

No comments:

Post a Comment