JAVA

Friday, October 16, 2015

HAWA NDIO DIVA'S WA BONGO WANAOTUMIA HASHTAG YA #WCW



#WCM ni Hashtag maarufu kwenye mitandaao ya kijamii ikamaanisha “woman crush  Wednesday” ziko nyingine kama  #MCM #TBT #LOL ni baadhi tu ya vifupisho watu wengi
hutumia katika mitandao ya kijaamii hasa Istagram, hapa tuangalie mastaa ya bongo ambao hashtag  ya #WCW inawafaa kila utapotamani kupost  #WCM basi kwa bongo nzima hawa wanabamba na wanastahili kutupiwa instagram na hashtag hiyo.
            
                                                        Jokate Mwegelo

    Aliwahi kushika nafasi ya pili Miss Tanzania 2006, Mwanamitindo, (Model), Msanii wa Filamu, mwanamuziki na MC (mshehereshaji), Kidoti ni jina la bidhaa za urembo ambazo ni maarufu sana kama nywele na viatu, ni mwanadada aliejidhatiti katika kujiendeleza kiuchumi na kusaidia vijana hasa wanafunzi katika kujiamni na kutunza vipaji.

                                                           Flavian Matata
Mwanamitindo, Miss universe Tanzania 2007 na mwanamitindo wa kwanza kutoka nyumbani Tanzania kushiriki miss Universe akiwa amenyoa kipara  na kuingia hadi 15 bora, na kushika nafasi ya 6.  Mwaka 2011 alipata tuzo  za Arise Magazine Lagos Nigeria kama mwanamitindo wa mwaka.

Jacqueline Ntuyabaliwe
Miss Tanzania 2000, Mwanamuziki wa zamani  pia ni Mke wa Bilionea Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Abraham Mengi. Pia ni mama wa watoto wawili mapacha. Wapo Mastaa wengine wengi wanaostahili  kupata #WCM ambao sija wataja hapo kama Wema Sepetu, Mwasiti Na wengine wengi.

Nancy Sumari
Miss Tanzania 2005, Miss world Africa 2005 Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Neghesti-Sumari Foundation  na ni mwanzilishi wa The Tanzania Women of Achievement Awards. Vile vile ni mwandishi wa kitabu cha “Nyota yako” 2013 kitabu maalum kwa watoto.

Vanessa Mdee
Vee money ni jina kubwa Tanzania kwa sasa, dada wa vipaji tele, mwandishi mtunzi, muimbaji, mtangazaji wa redio na Tv , ameshanyakuwa Tuzo 3 kutoka Kilimanjaro music award kwa miaka 3 mfululizo  2013- 2015. Alinyanyuka kidedea pia katika tuzo za AFRIMMA (African Muzik Magazine Awards) 2015 na kuchaguliwa kuwa mwanamuziki bora wa kike kutoka Africa mashariki.


No comments:

Post a Comment