Wiki hii stori ya soka ambayo inatawala sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa Bongo ni kile kitendo alichokifanya nahodha wa Mbeya City dhidi ya nahodha wa
Azam Fc walipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uwanja wa Azam Complex na Azam Fc walifanikiwa kuibuka na ushindi wa Magoli mawili kwa moja la Mbeya City.
Katika mchezo huo Juma Nyoso ambaye ndiye nahodha wa Mbeya City alimfanyia John Bocco kitendo ambacho sio cha kiungwana kwenye michezo na kupelekea mpaka mastaa kibao kufunguka.
Diamond Platnumz alipost picha na baadhi ya maneno kwenye account yake ya facebook;
'Wachezaji kama hawa ndio wanazidi kuitia Dosari na kulididimiza soka la Bongo na kufanya tuzidi kuonekana mambulula... Badala ya kupiga soka Unawaza kumtia mchezaji Mwenzio dole ili akipaniki apewe kadi Nyekundu Atolewe.... Kweli namna Hii Tutafika World Cup..??? -Diamond Platnumz
No comments:
Post a Comment